SHARE

Kawaida ya smatskills kukupa kitu bora kabisa kwenye simu na kompyuta yako. Leo tunakupa uchambuzi makini ni vivinjari gani vina faa na bora kwenye simu?

1.UC browser:-kwanini ni bora? Hiki kama umetumia huwezi kulinganisha na kivinjari chochote. kina sifa nyingi sana,sifa kuu ambayo kwengine haipatikanni ni kuhifadhi clipboard(kibao cha kunakili)hii ni kiboko ya matangazo,yani ukivinjari web zenye matangazo ya kufunuka kioo kizima(pop up)hichi ndo dawa yao.sifa zingine ni. ads blocker,pop up video player

hiki ni kizuri kwa kupakulia vitu,unaweza kupakua hata vitu 6 kwa wakati mmoja,kuendelea kupakua kama uliishiwa na data.

2.Chrome:-hichi kinatengenezwa na Google,kinakuja na simu nyingi za android isipokua yale matoleo ya China. faida ya kuwa na hiki ni kuhifadhi historia ya web ambazo ulitembelea,kuhifandhi nywila zako pia,kufungua tab nyingi uwezavyo pia,hata ukipoteza simu mambo yako utayakuta salama.

hiki ni kizuri kwa matumizi ya kawaida sana tena kwa mambo muhimu,kama mabloggers na watu wa kawaida pia.

3.Flynx:- sifa ya kwanza ya hichi ni chepesi na kiko fasta pia,faida kubwa ya kivinjari hichi ni uwezo wa kufungua kiungo popote bila kutoka eneo hilo, mfano umetumiwa kiungo ukiwa unachati whatsapp ukiwa na flynx unaweza kufungua na kusoma kilichopo ndani bila kutoka nje ya whatsapp,yaan huku unasoma huku unachati.

Kama hupendi usumbufu wa kutoka sehem moja kwa ajili ya kubrowse basi hiki kinakufaa sana.#

4.Pufin Web Browser:- kivinjari hiki ni muhimu sana kama huna kompyuta,ukiwa na simu yako kinakuwezesha kuvinjari kwa muonekano mzima wa web. Japo vingine vina uwezo wa kubadilisha ili kupata huduma hii kwa pufin hapa ni kawaida yake,unaweza kuset pia kama unataka kutumia mause au kawaida.

Kama unapenda kufungua website iwe na muonekano kama wa kompyuta basi pufin inakufaa zaidi kuliko nyingine.

5.Internet:- hii ilikua inakuja na simu za Samsung tu,lakini toka mwaka jana Samsung wameamua kuachia kwa vifaa vyote na sasa play store unaweza kupakua kwa urahisi tofauti na zamani.

kivinjaro hiki kina urahisi sana wa kushiriki,kubadili night mode[muonekano wa usiku],kubadili ukubwa wa maandishi,popup player n.k

Unahisi  kuna kivinjari kilichosahaulika hapo? karibu niambie kwenye komenti.

authenticaiton failed.
Facebook Comments