SHARE

Kampuni ya Google inazidi kutanua wigo kila nyanja,hii inatokana na huduma zao kupendwa na kutegemeka kwa kila mmoja.

Hapa ndio unaweza kusema “mwenye nacho atazidi kuongezewa” kwanini? Kupitia huduma yao ya YouTube Red inajikusanyia pesa kutoka kwa watumiaji watakaojiunga na huduma hiyo.

Ukiwa na YOUTUBE Red

INA TOFAUTI GANI NA YOUTUBE YA KAWAIDA?

  • Ukiwa na YouTube Red hutapata usumbufu wa matangazo yanayopatikana kwenye app ya kawaida
  • Ukiwa na YouTube Red utaona vipindi halisi vya tv,(yani siyo vya kurekodi)
  • Ukiwa na YouTube Red hutalazimika kutumia data kama app ya kawaida.
  • Ukiangalia video ni moja kwa moja hakuna tangazo katikati ya video.
  • Unaweza kutoka kwenye app na mziki wako ukaendelea kucheza bila kukata.

Hizo ni sifa chache za YouTube Red,hii huduma unalipia,na ili kumjali mteja wake unapewa huduma kwa mwezi mmoja bure, baada ya hapo ndipo uanze kukatwa pesa.

Tanzania huduma hii bado haijafika lakini itakuja hivi karibuni, Endelea kuwa na smatskills kwa habari zaidi.

authenticaiton failed.
Facebook Comments