SHARE
kama tunavyojua mitandao ya kijamii imekuwa na mchango mkubwa katika kuenea  kwa taarifa, kusaidia kutangaza biashara na faida nyingine lukuki na wakati mwingine mitandao ya kijamii hiyo hiyo imekuwa na kero zake mpaka inafikia hatua mtu kutaka kufuta akaunti yake moja kwa moja. Sasa leo nitakuelekeza hatua kwa hatua jinsi ya kufuta akaunti yako ya facebook moja kwa moja
  • Hatua ya kwanza Ingia kwenye akaunti yako kwa kutumia browser ya simu au kompyuta

  • Hatua ya pili ;Nenda kwenye ukurasa wa kufuta akaunti wa Facebook katika browser yako kwa kupitia link https://facebook.com/help/delete_account kwa kuiandika kwenye bar ya anwani na kubofya  ↵ au BOFYA HAPA

Ikiwa hujaingia moja kwa moja, ingiza anwani ya barua pepe au nambari ya simu na nenosiri la akaunti yako, kisha bofya Ingia. Ni kitufe cha bluu katikati ya ukurasa.

  • Hatua ya tatu : Bonyeza alama yakufuta Akaunti Yangu[delete]. Ni chini ya ujumbe wa onyo katikati ya ukurasa.

  • Hatua ya nne: Ingiza tena neno lako la siri na email/namba ya simu ili kuhakiki

  • Hatua ya tano: Utajaza captcha code utakazoziona kwenye kiboksi kitakachotokea. Hizi captcha code ni mchanganyiko wa herufi na namba kama zitakuwa hazionekani vizuri unaweza kujaribu tena kwa kubofya “try another text”

  • Hatua ya sita: Baada ya kuingiza captcha code utabofya OK kuendelea

Hatua ya mwisho utaulizwa kama uko tayari kufuta akaunti yako ya facebook moja kwa moja utabofya Ok kufuta akaunti yako.

Kama kuna sehemu umekwama au unamaoni unaweza kuniachia hapo chini

authenticaiton failed.
Facebook Comments