SHARE

JINSI YA KUTOA WRITTEN PROTECTION KWENYE DISK.

Jinsi ya Kuondoa written protection kwenye Disk, fungua Start menu, na bofya Run. andika regedit na ubonyeze enter. Hii itafungua registry editor.

Hatua inayofuata ni kwenda kwenye njia ifuatayo:

HKEY_LOCAL_MACHINE\SYSTEM\CurrentControlSet\

Bofya mara mbili kitufe cha write protect kilicho upande wa kulia na weka thamani ya 0.

Nenda kwenye Data Valuebox na ubofye OK: Kisha Restart Kompyuta yako.

NJIA YA #1 : JINSI YA KUTOA WRITTEN PROTECTION KWENYE USB FLASH & MICROSD CARD .

Jinsi ya Kurekebisha Written protection kwenye kadi yako ya Kumbu kumbu. madirisha Usajili kwa kufanya hatua zifuatazo:

– Fungua “START MENU” kama tulivyosema hapo awali. Andika “regedit” kisha bonyeza Kitufe cha enter. Bonyeza “yes” kufungua Registry Editor ya window.

– Kisha bofya mara mbili mouse yako kutoka Registry Editor, kisha jaribu kufikia njia hii “

HKEY_LOCAL_MACHINE \ SYSTEM \ CurrentControlSet \ Control \ StorageDevicePolicies “

– Baada ya kufikia njia hio, Angalia mahala hapa Registry key “writeProtect” kisha ubofye Right click “modify“, itafunguka na utaona thamani (value) muhimu 1 badili kwa iwe ziro kisha bonyeza OK.


#2 : JINSI YA KUTOA WRITTEN PROTECTION KWENYE USB FLASH & MICROSD CARD .

-update Usb flash drive yako “kwanza unatakiwa upate chip genius Usb flash yako hapa na maanisha Chip vindor kisha tafuta kwenye google kuhusu firmware ya usb flash driver yako ndipo ufanye sasisho

AU

Jaribu Programu zingine za kuformat usb flash yako kama Hp disk format toolna HDD low level format.


#3 : JINSI YA KUTOA WRITTEN PROTECTION KWENYE USB FLASH & MICROSD CARD

Tatua Tatizo hili kwa amri za DOS kama ifuatavyo:
– Kutoka Windows kuanza menu bonyeza RUN au unaweza kuonyesha kwa kubonyeza “kitufe cha Windows pamoja na kitufe cha R kutoka keyboard yako kisha andika CMD.

– Andika hii cmd “diskpart” Basi window itafungua sehemu mpya ambayo utabonyeza YES.
– Andika utaratibu huu “ list disk.” halafu bofya enter, DOS itaonyesha vifaa vya disk kwenye PC yako.

– Andika “select disk 2” kisha enter. Zingatia Chagua label ya usb flash au lebo ya microsd card kama ni disk 1 au 2.
– Andika “attributes disk clear readonly” kisha bonyeza enter.

“Baada ya Hapo chomoa Flash au Kadi yako ya Kumbukumbu kisha chomeka tena. “

kwa Kufanya Hivo Utaweza Kuondoa tatizo la write protections kwenye disk zako.

authenticaiton failed.
Facebook Comments