SHARE

Kama wewe ni mpenda soka na unafuatilia kwa makini toka kitambo kidogo kuna kitu utakuwa umegundua, Maandishi ya aina tofauti kila kombe la dunia.

Hapa kwa watundu wa simu wanaelewa sana FONT STYLE  hii ni aina ya maandishi au mwandiko. Kombe la dunia2018 kule Urusi mwandiko unaotumika unajulikana kama Dusha na mbunifu wake akiwa ni Brandia Central mwaka 2014 raia wa Ureno.

Mwandiko aina ya dusha maalum kwa kombe la dunia 2018 Urusi

Kwa upande wa kombe la dunia 2014 Brazil zilitumika Funny(jina siyo rasmi)

Funny zilitumika kule Brazil 2014

Kwa upande wa Afrika Kusini 2010 zilitumika aina hii ilijulikana kama SAF

Maandiko wa SAF maalum kwa kombe la dunia 2010

Kitu ambacho unaweza kuona ni kwamba zikishaanza kutumiwa hizi font utaziona kila sehemu,yaani kwanzia matangazo ya televisheni, kwenye mitandao na mambo yote yanayohusika na FIFA kwa wakati huo. Lakini baada ya hapo zinabuniwa nyingine tena.

Kama umezipenda unaweza kuzitumia kwenye simu yako kamakSamsung S8 kwenda lakini matoleo mengine ya android lazma uwe umeroot simu yako. Tumia app ya iFont kuiapply kwenye kifaa chako na hakikisha umezifungua kwanza mana zimefungwa mfumo wa zip na rar. Ukishafungua utaona zikiwa tff hizo

Pakua Dusha2018Urusi Pakua Funny2014Brazil

Kwa upande wa Afrika Kusini hazipatikani huenda labda kwa kuwa teknolojia ya sasa ilikua bado ndio maana hazikuweza kupatikana kaa matoleo ya simu yaani mfumo wa tff.

Kuna hatua itakayokushinda unaweza kuandika kwenye maoni chini hapo na utapata msaada haraka.

authenticaiton failed.
Facebook Comments