SHARE

Kila kukicha soko la simu janja linazidi kujaa  washindani. Kwa hiyo ukizubaa unaachwa na wajanja au wababe wa soko  kama Samsung,Sony,LG, iPhones na nyingine nyingi.

Mara hii tHL kwa mara ya kwanza inaleta simu yao sokoni, kulingana na ukurasa wa kampuni hiyo kwenye facebook wametangaza kuwa kwanzia juni 1 wataachia simu hiyo inayoonekana ya ajabu kulingana na sifa zake.

tHL NI NINI?

Hii ni kampuni inayomiliki app maalum na ya kitanzania kutoa madokezo kwa wanafunzi,kwanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. App ipo kwenye masoko yote kwanzia simu janja hadi kompyuta.

Mionekano mbalimbali ya simu aina ya thl

SIFA NA UWEZO WAKE.

  • Wireless charging capability(Ina uwezo wa ku-charge bila kuchomeka cable),
  • Camera yake inafanya kazi kwa mtindo wa jicho la binadamu linavyofanya kazi(Nyuma ina (13+5)MP na mbele 8MP)
  • Ina RAM 4GB
  •  Storage ina 64GB(Na unaweza kuongeza mpaka 512GB)
  •  Android yake itakuja na  7.0 Nougat iliyoboreshwa
  • Battery 4200mAh na ina uwezo wa FAST charging ndani ya dakika 5 ina-charge 6% na unasubiri muda kidogo tu simu inajaa. Pia inakaa na charge kwa zaidi ya saa 30.
  • Screen yake ni 6 inch 1440*720Pixel HD+ 18:9 Aspect ratio, 9. In finger print.
  • Unaweza pia kufungua kwa sura yako(FACE recognition.)
  • Inaingia laini 2 za 4G LTE, pia unaweza kuitumia kwenye 3G na 2G.
  • Frame yake ni ya chuma kwa ajili ya usalama wa simu ikitokea ikianguka,na nyingine nyingi.

Hakika hii simu ni ya kipekee saba,wewe kama msomaji unaumaoni gani kuhusu ujio wa simu hii?na kitu gani muhimu cha kuzingatia ili kampuni mpya au changa itusue kwenye soko?