SHARE

YouTube inatoa chombo kwa wabunifu ambao wataangalia ili kuona kama video zao zimeibiwa. Sasa, kila wakati video inapakiwa kwenye YouTube, huduma ya chombo hicho itasoma na kuangalia kama maudhui tayari yalishawekwa au yanafanana na video nyingine kwenye tovuti. Sio Itakuwa inatambua clips pia hata video kamili.

Chombo, ambacho YouTube inakiita Copyright Match tool kitatolewa kwa wenye channel na walio na wanachama (subsribers)zaidi ya 100,000 kuanzia wiki ijayo. Itasambazwa kwa watumiaji zaidi katika miezi michache ijayo. Waumbaji wanaotumia chombo watafahamishwa kama nakala za video zao zitaibiwa na kuwekwa tena kwenye YouTube. Ikiwa chombo kikinasa video basi mtengenezaji anaweza kuamua hatua ya kuchukua. anaweza kufanya chochote, kuwasiliana na mtu aliyefanya kuiba nakala hiyo, au aombe YouTube kuondoa nakala hiyo.

authenticaiton failed.
Facebook Comments